Mzalendo.net
--2012 NOV 8
播放聲音
喜歡
評論
分享

詳細信息

Novemba 5 visiwa vya Zanzibar viliadhimisha mwaka wa pili tangu kuundwa serikali ya Umoja wa kitaifa kati ya chama cha mapinduzi CCM na kile cha wananchi CUF, Hatua hiyo ilitokana na matakwa ya wananchi. Kuundwa kwa serikali hiyo ya mseto baada ya uchaguzi mkuu uliopita 2010, kulitokana uamuzi wa wakaazi wa visiwa hivyo katika kura ya maoni ilioitishwa kama sehemu ya maridhiano yaliofikiwa baina ya aliyekuwa Rais wa Zanzibar wakati huo Amani Karume na Katibu mkuu wa chama cha CUF Maalim Seif Sharif Hamadi. Katika kipindi hiki cha Kinaga ubaga Mohammed Abdulrahman amefanya mahojiano na Makamu wa kwanza wa Rais wa serikali yamapinduzi ya Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamadi ambae pia ni Katibu Mkuu wa CUF.

查看更多